0
Vanessa Mdee amesema pamoja na kuondoka B’Hits Music Group, bado uhusiano wake na label hiyo upo vizuri.

Akiongea kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, Vanessa alisema bado anamchukulia Hermy B kama kaka yake.

“Tuko vizuri sana, Hermy ni rafiki yangu, ni kaka yangu hata nikihitaji ushauri leo naweza nikampigia na hatokuwa na shida ya kunipa ushauri kwahiyo you know he is my good friend mkataba wetu ulifikia tu tamati,” alisema.

Vanessa alikuwa nchini Kenya kwenye media tour.

Post a Comment

 
Top