Lady Jaydee amesema wakenya wengi wanadhani yeye pia ni mkenya na kwamba kabila lake ni mkikuyu.
Jide ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa kila anapokuwa kwenye show nchini humo, mashabiki wake humtaka ahamie nchini humo moja kwa moja.
“Unajua Wakenya wamekuwa wakisema mimi ni Mkikuyu, wanadai natakiwa nikaishi nchini kwao wanajua mi ni Mkikuyu ila nawaeleza ukweli ni kwamba naipenda Kenya, lakini mimi ni Mtanzania na daima nitaipenda nchi yangu,” alisema Jaydee.
Katika hatua nyingine Lady Jaydee anajiandaa kushirikiana kwa mara nyingine na msanii wa mwenye asili ya Burundi, Kidum.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment