Inadaiwa baada ya Karrueche kuona hivyo alichukia na kuamua kuondoka, na Chris naye akamfata nyuma kuelekea kwenye gari yake.
Vyanzo vya karibu na Karrueche vimedai kuwa Chris baada ya kukataliwa kuingia kwenye gari ya mrembo huyo alimfata hadi nyumbani kwake mida ya saa tisa na nusu usiku, na kuanza kumgongea mlango huku akipiga makelele pamoja na washikaji zake alioongozana nao.
Hata hivyo Karrueche aliondoka nyumbani kwake na kuelekea kwenye mgahawa mmoja ambapo Brown alimfata tena baada ya muda, na wakiwa ndani walisikika wakibishana kwa sauti kabla ya Karrueche kuamua kuondoka na kurudi nyumbani bila Chris.
Mapenzi ya wawili hao yalifika ukingoni baada Karrueche Tran kumpiga chini Breezy baada kugundua kuwa ana mtoto na mwanamke mwingine ambaye hakuwahi kumwambia.
Post a Comment