0
Rapper Juma Mchopanga a.k.a Jay Moe amesema kuwa mapokeo ya single mpya anazotarajia kuanza kuzitoa hivi karibuni ndio yatakayompa uhakika wa lini atatoa album mpya.
Jay Moe ambaye amekaa muda mrefu bila kutoa nyimbo wala video, amesema kuwa mwezi huu wa sita anatarajia kuachia single mpya pamoja na video.

“Nadhani tutaanza kutoa singles, ndani ya huu mwezi wa sita tunaweza kuanza kurelease single ya kwanza ya pili, video yake ukizingatia watu wamekaa muda mrefu bila kuona video ya Jay Moe, kwahiyo nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri sana kuweza kurudi.” Alisema Jay Moe kupitia E-Newz ya EATV.

“Kwahiyo baada ya hapo respond ikiwa nzuri kurelease album ambayo tayari unayo sio kazi, kazi ni kutoa singles watu wakazikubali tayari kuinunua hiyo album.”

“Nadhani kwanza album itategemea na respond nzuri ambayo itatoka kwenye singles ambazo ntaachia. Kuna nyimbo tatu, nne, tano kali sana nimezirekodi kwenye nyimbo zaidi ya ishirini, kwahiyo tumepick zile kali zile kila mtu akisikia anasema yeah hii hapa inaweza ikakurudisha vizuri.” Alimaliza Jay Moe.

Post a Comment

 
Top