0
Baraza la Sanaa Taifa, BASATA, limesema kitendo cha wasanii kutoa wimbo mmoja badala ya album iliyokamilika kinawapa ugumu wa kukagua kazi hizo.
Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Afisa habari wa BASATA, Aristide Kwizera alisema wanachoweza kufanya ni kuhakiki kazi zilizopo kwenye album.

“Kwa sasa hivi kazi ambazo zinahakikiwa ni zile ambazo zipo kwenye mfumo wa album. Lakini inapokuwa ni single, bado mechanism hii haigusi eneo hilo. Urasimishaji haugusi kuikagua single moja moja. Utaona kwamba sasa hivi wasanii wa muziki wa kizazi kipya, wengi hawatoi album, wamekuwa watu wanaotengeneza single moja moja, anatafuta show na ndio pato lake linatokea kwenye hiyo single,” am Kwizera.

“Msanii anapaswa kusajiliwa na baraza la sanaa la taifa ili kwanza atambuliwe kuwa ni msanii na anafanya kazi za sanaa. Kwa sasa hivi baada ya serikali kurasimisha sekta ya sanaa, msanii yeyote kabla hajapeleka album yake sokoni, ni lazima kazi yake ihakikiwe na BASATA kwa wale wanaofanya muziki. Kwa wale wanaofanya filamu kazi zao inabidi zihakikiwe na bodi ya filamu, pamoja na video zinazozalishwa na wasanii wa muziki. Kwahiyo msanii anapotoa video kazi zake lazima zihakikiwe na bodi ya filamu na audio ni lazima ihakikiwe na baraza la sanaa la taifa.”

Post a Comment

 
Top