
Diamond ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa tuzo ya MTV EMA ‘Best Worldwide Act Afrika/India’, amesema anafikiria kushoot video hiyo nchini Marekani pamoja na Africa.
Ne-Yo ambaye alikutana na kufanya kazi na Diamond wakati wa Coke Studio Africa jijini Nairobi, Kenya alikuwa miongoni mwa mastaa waliompongeza Baba Tiffah kwa ushindi wa MTV EMA kupitia Instagram kwa kuandika, “CONGRATS TO MY HOMMIE @diamondplatnumz for winning #BestWorldWideAct at the #MTVEMAs keep being great! Let’s go get em’ my guy!”
Post a Comment