0

Hit maker wa “Tunda langu” kutoka Mbeya Ammy Chiba aliyomshirikisha msanii Barnaba amesema kuwa

Januari 2016 anarudi rasmi kwenye game kwa kuachia single mbili zenye mahadhi tofauti ya muziki.

Akiongea kwenye mahojiano na Ergon Elly katika kipindi cha 97 Show cha Redio Kitulo Fm Mkoani Njombe,Ammy Chiba amesema kuwa alikuwa kimya kutokana na jukumu la kulea mtoto wake Alvin (miezi 2) ambae ndio motto wake wa kwanza na wa pekee.


“Uongozi wangu tayari umeandaa mpango wa mimi kufanya kazi mbili siku chache zijazo kuanzia sasa katika studio kubwa hapa nchini na ifikapo januari 2016 kazi ni kuzi-push kwenye Media kubwa na ndogo”.


Wakati huo huo Ammy Chiba amezungumzia changamoto ya kazi zake kutofanya vizuri maeneo mengine kama mikoa ya kusini ambapo amesema kuwa Media karibu zote nchini uongozi wake unasambaza| kuzipeleka lakini changamoto ni fedha kwani watangazaji wengi wataka kulipwa nyingi ndipo wacheze kazi za msanii.


“Watangazaji/Media wanahitaji kulipwa fedha nyingi ili kucheza kazi zetu ili hali sisi bado ndio tunachipukia katika muziki na misingi ya kupatia pesa kama vile shows bado haijaimarika na hata kama wadau wa media wakichagua kazi zetu bado kupewa nafasi ya kusikika ni ndogo tofauti na wasanii wakubwa”.
Sikiliza full Interview hapa

Post a Comment

 
Top