0
 
Hit maker wa Nimepania na Balling and Chilling Sam Misago amesema kuwa awali aliwahi kufanya
muziki kwa muda wa mwaka mmoja kabla hajawa mtangazaji wa Redio na Runinga.

Kwenye Mahojia na Mtangazaji Ergon Elly wa 97.1MHz Njombe Tanzania Sam Misago amesema katika Kipindi ambacho alikuwa anajishughulisha na movement za muziki alifanya nyimbo mbili ambazo alisaidiwa kuandika mashairi na kurekodi studio na Rapper JCB.


Na baada ya kuingia kwenye taaluma ya utangazaji Sam aliendelea kuandika nyimbo mbalimbali ingawa hakuwahi kuingia studio kurekodi nyimbo mpaka alipoamua mwaka huu kurudi rasmi kwenye game kwa kurekodi wimbo wake wa kwanza aliomshirikisha mfalme wa RnB Tanzania Ben Pol “Nimepania” ambao tayari video ya wimbo huu imeshatoka.


Sikiliza Mahojiano hapa “Sam Misago na Ergon Elly”

Post a Comment

 
Top