0

Staa wa kike anayetikisa kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva na Bongo muvi zuwena Mohamedi maarufu kama shilole ambaye hivi karibuni ameachana na aliyekuwa

mpenzi wake ambaye pia ni mwimbaji wa Bongo fleva Nuh Mziwanda,amefunguka na kusema licha ya mahusiano yake kwenda kombo na staa huyo wa “Bilima” bado yuko
‘happy’ na hana hata punje ya ‘stress’. 


Shilole amefunguka hayo baada ya kuwepo na tetesi kwamba amekuwa akinywa pombe kupindukia ili kupoteza mawazo yanayotokana na kuvunjika kwa uhusiano wake na Nuh. Shilole pia amekana kuwa na uhusiano na rapa BillNas na mwimbaji Bonge la Nyau(sasa hivi Nyauloso) kama ambavyo ilikuwa inahisiwa kuwa anaweza kuwa 


anatoka na mmoja kati ya mastaa hao.Hakuishia hapo mwanadada huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa nyang’anyang’a amekana pia kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja(usagaji). 


Shilole amesema kuwa haoni haja ya watu kuanza kuzusha zusha nani anatoka naye,atamweka hadharani mwenyewe akitaka japo amedai kwa sasa hana mpango na mapenzi yupo kikazi zaidi

Post a Comment

 
Top