Mwanzilishi wa kundi la muziki Wanaume Family na Yamoto Band, Said
Fella amesema kama msanii anataka kufanya muziki, lazima yeye au uongozi
unaomsimamia wawekeze fedha kwenye muziki wake.
Fella amewataka wasanii kuacha kuupeleka muziki wao kishkaji shkaji na waonyeshe nia ya dhati kwenye muziki wao.
“Kila msanii ana malengo na muziki anaoufanya, ukiamua kuwa
mwanamuziki kampuni lazima utie pesa’, yaani uamue kabisa ngoja nifanye
muziki fulani. Maana ya pesa sio lazima uwe na milioni kumi, milioni
ishirini. Ni useme ‘mimi sitaki mwana Marco Chali anitengenezee beat
bure au Adam Juma anifanyie video bure kishkaji shikaji tu. Yaani Adam
Juma akisema milioni nne mpe milioni nne akufanyie kazi yako. Marco
Chali akisema beat laki tano mpe laki tano yake afanye kazi yake. Mpaka
hapo ndo tutakuwa tumejiweza kufanya biashara ya muziki, kufanya muziki
ule wa kampuni,” amesema Fella.
“Kikubwa kila msanii anatakiwa kuwa na nia na achokifanya,”
ameongeza. “Kwa sababu mwisho wa siku kila msanii anatakiwa kutambua
anafanya muziki gani? Huu muziki ninaofanya ni wa biashara au la? Au
muziki wa maendeleo. Ukifanya muziki wa kikampuni ina maana sitaki tena
nidondoke. Kwahiyo lazima utakuwa unatengeneza muziki wako pamoja na
maisha yako.”
“Lakini kuna watu wengine wanafanya muziki lakini hawana malengo kama
hayo niliyoyasema, wana malengo mengine wanayoyafikiria. Wengine
wanasema nikipata pesa ninunue gani, wengine ninunue nyumba kila mmoja
ana malengo yake. Kwahiyo lazima ujitambue muziki gani unataka kufanya.
Hata mimi sikumwambia Master Jay kwamba muziki anaoufanya Shaa ni
mbaya, ila nilimwambia kuna muziki akifanya Shaa mafanikio yatakuwepo,
kwamba huyu anafanya ndiyo lakini wanasikiliza matajiri lakini tajiri
atasikiliza muziki wakati yupo kwenye gari, atasikiliza muziki kama
ataenda kwenye kumbi za starehe. Lakini akiwa ofisini kwake ataangalia
muziki wa Ulaya tu, hafikirii muda wote kwamba atasikiliza muziki wa
fulani. Lakini kuna watu wanasikiliza muziki huo muda wote na ndo kama
maisha yao. Ndio maana Shaa akaamua kufanya muziki unaopendwa na watu
wengi.”
Home
»
Entertainment
»
GOSSIP
»
MUSIC
» Said Fella: Bila kuwekeza fedha kwenye muziki msanii unapoteza tu muda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment