0
Mama mzazi wa rapper wa kike Onika Tanya “Nicki Minaj” Maraj aitwaye Carol Maraj, ametoa majibu ya maswali yaliyoibuka wiki iliyopita kama ni kweli rapper Meek Mill amemchumbia Nicki Minaj ama laa.
Carol Maraj amesema kuwa huwa anazungumza na binti yake kila siku, na amemhakikishia kuwa hajachumbiwa na Meek Mill.

“I talk to my daughter everyday, and she said she was not engaged,” aliiambia Bossip.



Uvumi huo ulianza baada ya Nicki Minaj kupost picha ya mkono wake wa kushoto Instagram inayoonesha pete ya almasi yenye umbo la moyo kwenye kidole chake cha chanda..

Post a Comment

 
Top