0
Mkali wa ‘Latifa’, ‘Mapenzi kitu gani’, ‘Si uliniambia’ na nyingine nyingi, Mbwana Mohamed a.k.a MB DOG amesema licha ya muziki kuwa na ushindani mkubwa lakini bado anajaribu kufanya jitihada za kuirudisha nafasi aliyokuwanayo kwenye muziki.
MB Dog amesema bado ana nafasi kubwa ya kurudi na kulishika soko kama zamani.

“Nafasi ninayo kubwa sana, nipo katika harakati za kuirudisha heshima yangu, 100% uwezo ninao, sasa hivi wasanii ni wengi na silaha ambayo wanaitumia ni kuji-promote, ndo maana hata mimi sasa hivi naji-promote kadri ya uwezo wangu, kwahiyo sasa hivi kuna mambo mengi wa kiutandawazi, kwahiyo na wewe unatakiwa kwenda nao sambamba kwa kujitangaza na ujanja ujanja wa kuongea na wanahabari na vitu kama hivyo, kwahiyo muziki wa sasa hivi nguvu inaitajika sana kwenye ku-promote kazi,” alisema MB Dog.

Post a Comment

 
Top