0
G-Nako huenda akawa ni miongoni mwa wasanii waliofanya collabo nyingi zaidi mwaka jana lakini hiyo imeanza kumpa wasiwasi. Rapper huyo wa kundi la Weusi anahisi ameanza kuwachosha mashabiki na hivyo ameiambia Bongo5 kuwa atajitahidi kuangalia njia gani bora atafanya ili asiwachoshe mashabiki wake.

“Bado naendelea kuchajisha collabo lakini sasa hivi sitafanya collabo nyingi sana,” amesema. “Sometimes unajua ukifanya collabo nyingi unawachosha mashabiki wako. Kama mimi nimeshafanya nyingi, kwahiyo sasa hivi kuna kazi nitakuwa naangalia za kufanya na zingine zitafanya kwa sababu collabo zimekuwa nyingi sana kama naona watu wametosha hivi na collabo.”

Post a Comment

 
Top