Kutokana na vurugu zilizozuka wiki hii huko Afrika Kusini kutokana na raia wa nchi hiyo kuwashambulia na kupora mali kwenye maduka yanayomilikiwa na raia wa kigeni, kituo cha radio cha Q FM cha Zambia kimesitisha kupiga nyimbo za wasanii wa Afrika Kusini kwa lengo la kupinga mashambulizi hayo.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Asan Nyama amesema kuwa wamefanya uamuzi huo ili kuungana na Waafrika kutoka nchi zingine waliokumbwa na vurugu hizo jijini Durban, Afrika Kusini.
Nyama amesema kuwa QFM imesikitishwa na vifo vya watu watano wa mataifa ya nje waliopoteza Maisha baada ya kushambuliwa na wananchi wa Afika Kusini. Mkurugenzi huyo amesisitiza umuhimu wa raia wa nchi mbalimbali Afrika kuishi Kama ndugu na kuomba serikali ya Afrika Kusini kukabiliana na unyama huo.
Chanzo: Mseto EA
Home
»
Entertainment
»
STORY
» Radio ya Zambia yasitisha kupiga muziki wa Afrika Kusini kupinga mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment