0
Hali ya ubaguzi na ukatili dhidi ya raia wa kigeni wanaoishi nchini Afrika Kusini inazidi kuiweka nchi hiyo kwenye wakati mgumu wa kutengwa na nchi zingine za Afrika.
Tayari baadhi ya nchi zikiwemo Zimbabwe na Zambia zimetangaza kusitisha kucheza nyimbo za wasanii wa Afrika Kusini.

Tanzania tunaweza kufanya hivyo pia? Bonta ana mtazamo tofauti.

Rapper huyo wa Weusi anaamini kuwa tukisitisha kucheza ngoma za wasanii wa South wapo wasanii kibao wa Tanzani ambao nao wataathirika kwakuwa nyimbo zao zina ladha za nchi hiyo.

Akiweka picha Askofu Desmond Tutu, Bonta ameandika kwenye Instagram:

Heshma yako baba Ni kweli mmesahau jinsi tulivyowasaidia kipindi cha APARTHEID POLICY????? Kweli mnauwa ndugu zenu na kuwakumbatia na kuishi nao bABILOn ambao kiukweli ndio waliochukua mKATe wenu!!!! Naskia vituo vya redio MALAWI NA ZAMBIA vimesitisha kucheza mziki wa SA!!! sijasema na sisi tusitishe coz tayari wasanii wetu majority wanafanya mziki wa Nigeria na SA, SO kusitisha kuucheza maana yake itabidi tusitishe kucheza na za wasanii wetu zenye mahadhi hayo!!! Teh teh tusifike huko coz alwayz hatunaga cha kwetu!!! XENOPHOBIA

Post a Comment

 
Top