0
Wiki moja tu baada ya kushinda tuzo ya mtumbuizaji bora wa Afrika kwenye MTV MAMA, Diamond Platnumz ameshinda tuzo nyingine kubwa ya Afrika.
Usiku wa jana, Diamond alishinda tuzo ya Msanii wa Afrika wa Mwaka kwenye hafla ya tuzo za African Achievers Awards 2015 zilizofanyika Afrika Kusini.
 “Thanks God for keep Blessing my Hustle….AFRICAN ARTISTE OF THE YEAR #AfricanAchieversAwards2015 (Shukran Nyingi ziwafikie Uongozi wangu kwa kuhakikisha unanisimamia ipaswavyo, Mama yangu kipenzi Sandrah, My beautiful Baby @zarithebosslady , Media zote, na Mashabiki zangu pendwa kwa kuendelea Kunisuport bega kwa bega,” ameandika Diamond kwenye Instagram.

“Pia Nimpongeze Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa Kushinda katika Tunzo hizi za #AfricanAchieversAwards2015 leo kama Kiongozi Bora wa Africa…. #MsaniiBoraAfrica #KiongoziBoraWaAfrica.”

Post a Comment

 
Top