Divina ampigia goti Mama Kanumba.. Kisaa!!!!
MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’, amesema anamuomba radhi
mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kwa kutofika kwenye uzinduzi wa kitabu cha marehemu mwanaye kutokana na taarifa hiyo kutomfikia mapema.
Davina alikiri kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao walikuwa karibu sana na marehemu enzi za uhai wake, akasema anaweza kuwa amekosea kwa namna moja au nyingine lakini kikubwa ni kwamba alipata taarifa muda ukiwa tayari umeenda.
“Ni kweli naweza kuchukua lawama kwa upande wangu, namuomba mama yangu anisamehe kwa sababu nilichelewa kupata taarifa nilipompigia Maya kumbe ndiyo muda huo uzinduzi unafanyika,” alisema Davina.
Uzinduzi wa kitabu cha marehemu Kanumba kiitwacho The Great Fallen Tree ulifanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Landmark, Ubungo jijini Dar
Post a Comment