0
 

Ni kama wiki sita hivi zimepita tangu kumekuwa na tetesi za kwamba
ndoa ya mastaa wawili, Mariah Careh na Nick Cannon imevunjika.

Story iliyoanza kuenea mitandaoni kuhusu wanandoa hao toka jana iko hivi, Nick Cannon ameandika talaka na yuko kwenye taratibu za kuachana na aliyekuwa mkewe, Mariah Carey.

 

Cannon amewashangaza mashabiki wake baada ya kuchukua uamuzi huo, japo hii inaweza kumpa wakati mgumu Mariah ambaye mara zote ni kama alikuwa akiamini watarudiana na Nick.



Mariah Carey huenda hii ikamuumiza zaidi, aliwahi kusema kuwa hapendi kuona watoto wao mapacha Monroe na Morrocan wanaishi maisha ya kulelewa na mzazi mmoja, japo Nick alionyesha nia ya kuendelea kuwahudumia kwa kila kitu.

Post a Comment

 
Top