0


Huu unaweza kuwa mwaka wa mafanikio zaidi kwa mastaa wengi Tz, tumeona Jokate akisign deal ya kufanya biashara kubwa itakayomzalishia zaidi ya bil 8 za kitanzania chini ya lebo ya Kidoti, safari hii ni zamu ya staa mwingine, Vanessa Mdee leo kuna story nzuri inayomhusu mtu wangu!


Kampuni ya Samsung ni kampuni maarufu kwa kuuza bidhaa mbalimbali, simu za mkononi ni moja ya bidhaa hizo, leo January 16 Vee Money ameingia mkataba wa kuwa Balozi wa bidhaa za Samsung.

Vanessa na uongozi wa kampuni ya Samsung wameingia makubaliano rasmi ya kufanya kazi pamoja, staa huyo ataanza kuonekana kwenye matangazo ya bidhaa za kampuni hiyo.

”Samsung ni kampuni kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa Balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya Kieletroniki ulimwenguni , huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015 utakavyokuwa na mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung, binafsi natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi“– Vanessa Mdee.




Post a Comment

 
Top