Ni Maria Carey na surprise hii kwa mashabiki wake Las Vegas…
Huu ni ubunifu ambao hata mimi umenivutia, nakumbuka mwaka 2012 rapper Jay Z aliwahi
pia kusurprise kwa kuingia kwenye treni ya abiria halafu akaendelea na safari, huku aliyekaa naye kiti kimoja alikuwa bibi mzee ambaye hata hakujua kwamba amekaa na staa mkubwa duniani!
Maria Carey naye amekuja na hii kwa fans wake Las Vegas, mashabiki wake walikuwa wakihojiwa ndani ya vyumba vya hoteli, wakaeleza namna ambavyo wanamkubali staa huyo, halafu ghafla mlango unagongwa na mtu ambaye anajitambulisha kuwa ni mhudumu wa hoteli, halafu wanapogeuka kumuangalia mhudumu wanakuta mhudumu huyo ni Maria Carey mwenyewe!
Hii imenivutia, katika surprise hiyo fans wake hao walipata nafasi ya shavu la ticket za show yake ambayo ataifanya May 6 Las Vegas, Marekani.
“Hili ni tukio muhimu kwangu na tena nina imani mashabiki wangu wataifurahia hii kwa sababu naenda kufanya shoo ambayo ni kama njia ya kuiongoza album yangu ambayo ni toleo la 18, naamini watu wengine watafurahia kwa sababu sijawahi kufanya hivi kabla“ — Mariah Carey.
Post a Comment