T-Pain wa Marekani kuja Tanzania mwezi ujao
Mfalme wa Auto-Tune, T-Pain kutoka Marekani anatarajia kuja Tanzania mwezi ujao na kutumbuiza jijini Mwanza, kwenye tamasha la uzinduzi wa radio mpya iitwayo Jembe Fm ya jijini humo.
T-Pain ambaye jina lake halisi ni Faheem Rashad Najm, hatakuwa peke yake kwenye tamasha hilo lililopewa jina la Step Up, bali atakuwa na msanii mwenyeji wake Diamond Platnumz. Show hiyo itafanyika February 21 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
“MWANZA!!! Get ready for the #STEPUP2015…. Kwa mara ya Kwanza Kabisa!!!, Hapa MONDI hapa NAPPY BOY! @Tpain you Better save the Date!..21| 02 |2015″ Diamond ameandika Instagram T-Pain ni mwanzilishi wa label ya Nappy Boy Entertainment iliyoanzishwa 2005. November 21, 2014 aliachia single mpya “Coming Home” kutoka kwenye album yake mpya na ya tano “Stoicville” ambayo bado haijatoka
Post a Comment