0
 
Vanessa Mdee a.k.a Vee Money amekuwa mwanamuziki wa
pili Tanzania kupata akaunti ya VEVO kwaajili ya kuweka video zake.


VEVO ni mtandao mkubwa namba moja duniani unaohusika kuhifadhi na kurusha kazi za wanamuziki maarufu duniani kama kina Nicki Minaj, Beyonce, Jay Z na wengine.

Gosby ndiye alikuwa msanii wa kwanza wa kizazi kipya kupata akaunti kwenye mtandao huo unaomilikiwa na kampuni kubwa za muziki duniani Universal Music Group (UMG), Google, Sony Music Entertainment (SME) na Abu Dhabi Media.

Wanamuziki wengi wa Afrika Kusini na Nigeria kama Mafikizolo, D’Banj tayari wana akaunti kwenye mtandao wa Vevo.

Post a Comment

 
Top