MAKUBWA YA GADNER YAFICHUKA
Wiki hii Lady Jaydee amewapa nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali naye kuyajibu kupitia akaunti yake ya Instagram. Ameulizwa maswali mengi, na miongoni mwa maswali hayo ni la kuhusu ndoa yake na mtangazaji wa Radio E-FM Gadner G. Habash.
Haya ni maswali na majibu kama alivyopost Instagram.
“Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?
JIBU : Hatuja achana niliamua kumuacha
Kwanini umeachana/umemuacha mume?
JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa
Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo. .. ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo , sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii. Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume? JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshma zaidi kuishi na mume asie na heshma, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba.
Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini . Ukiachilia mbali vipigo.
Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao. …..niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso.
Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?
JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi
Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.
Kwanini usirudiane na mumeo?
JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpk kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. …
When i say never, I mean Never.
Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?
JIBU : Nilidhani angebadikika, so nilikuwa natoa nafasi.
Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.
Uliwezaje kuondoka?
JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu.
Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima km kweli ntaweza ku move on?
Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpk muda huu nnapo type na ku post haya majibu.
Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga.
Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.”
Post a Comment