0
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ameanza kushoot video ya wimbo wake mpya ‘Njoo Uichukue’ ndani ya uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam pamoja na sehemu nyingine.

Mpoto akiimba

Akizungumza na Bongo5 leo msemaji wa Mpoto Theatre Gallery Ltd , Dominic Kaunda, alisema ndani ya video hiyo inayofanyWa na director Adam Juma wamewatumia Kitale na Stan Bakora ili waigize kama ni wazee wa uswazi.

“Tunashukuru mungu kazi imeenda poa, tumemaliza kushoot video na Adam juma na baada ya kama wiki moja itatoka,” amesema. “Tumetumia gharama kubwa kidogo kwa sababu tumekodi uwanja wa taifa kutwa nzima, tumewalipa wale jamaa wa mkude simba, irector Adam Juma pamoja watu ambao wataonekana kwenye hiyo video. Kwahiyo ni gharama kubwa kidogo sema siwezi itaja kwa sasa kwa sababu hivi ni vitu vya ndani ya kampuni. Tumejifunza sasa kuacha kuropoka kuhusu gharama tulizotumia tunataka watu waangalie ubora wa kazi.”


Kitale akiwa location


Mpoto akiwa mtaani katika hatua za kushoot video


Mpoto akiwa na Adam Juma ndani ya uwanja wa taifa


Mpoto, Kitale, Stan Bakora

Mpoto




Post a Comment

 
Top