0

MSANII wa filamu Bongo, Tiko Hassan ‘Tiko’, amefunguka kuwa anashindwa kuolewa kutokana na kukosa mwanaume

wa kufanya hivyo, ila yupo tayari kupokea barua ya uchumba kutoka kwa mwanaume yeyote atakayehitaji kufunga naye ndoa.
 

Msanii wa filamu Bongo, Tiko Hassan ‘Tiko’. Akimwaga ubuyu na Uwazi, Tiko alisema bado hajapata yule ambaye anaweza kuwa mume wake hadi sasa japo amesubiri kwa kipindi kirefu.
“Akitokea mwanaume na kuja kutoa barua nyumbani hata leo, nipo tayari na naweza kuishi naye lakini haina maana kwamba kila mwanaume anaweza kuja kwetu na kufanya hivyo. Mwanaume ambaye atakuja anatakiwa awe anajitambua ili tuweze kujenga familia,” alisema Tiko.

Post a Comment

 
Top