Dume Suruali ya Mwana FA huwenda ukawa ndiyo wimbo wa kwanza wa rapper huyo kufikisha views milioni 2 kupitia mtandao video wa YouTube kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Rapper huyo amedai sio kitu cha kawaida katika muziki wake ingawa kuna baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakifikisha idadi hiyo ya views kwa muda mchache.
“Najua najua, kwamba sio namba kubwa hii kwa baadhi ya wasanii,actually ni kanamba flani kaduchu tu,ila kwangu its a big deal..kwa hivyo sitakaa niigize hapa kuwa ‘this is how we do it’ na ‘it’s normal’,no it’s not,sio kawaida, nashangaa, asanteni sana,”. aliandika Mwana FA Instagram.
Aliongeza”how about tukifika 3m tunatoa ngoma nyingine?n ow lets get to 3m. shukrani sana!…Nawaombea Wiki Njema Mahangaikoni… #DumeSuruali
Faaaalsafa!,”
Wimbo huo aliomshirikisha Vanessa Mdee ni moja kati wimbo ambazo zimetokea kupendwa zaidi na vijana wengi kutokana na mashairi ya wimbo huo.
Home
»
Dj Speed | story | Teamkazi Enter|
» Story:Dume Suruali ya Mwana FA yafikisha views milioni 2 YouTube
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment