0
Muigizaji Angelina Jolie ameondolewa ovary zake pamoja na fallopian tube (mirija ya kupitia mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye nyumba ya uzazi) kama njia ya kujikinga na saratani.
Akiandika kwenye gazeti la New York Times, Jolie alisema alifanyiwa upasuaji wiki iliyopita kwakuwa ana gene inayomfanya awe na asilimia 50 ya kupata satarani ya kizazi.

Miaka miwili iliyopita, muigizaji huyo ambaye mama yake alifariki kwa saratani alifanyiwa upasuaji mwingine.

“It is not easy to make these decisions. But it is possible to take control and tackle head-on any health issue,” alisema.

Angelina na mume wake Brad Pitt wana watoto sita.

Post a Comment

 
Top