Kwa mujibu wa Atlas, kampuni moja ilimpa ofa hiyo Diamond ambaye hata hivyo alikataa.
Akiongea kwenye kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Atlas alidai kuwa hiyo ilionesha ni kiasi gani Diamond ana msimamo kwakuwa anajua kwa sasa kila mtu anamfahamu nchini humo na anaweza kupata fedha nyingi zaidi ya hizo.
Hata hivyo meneja wa Diamond, Salam amekanusha msanii wake kukataa kiasi hicho cha fedha.
“Hakuna show iliyokataliwa ila tulikuwa tunaongea na middle man sasa sijui yeye aliwaambia waandaji kiasi gani, plus walikuwa wanataka club appearance na show the next day kwa bei ya show peke yake kwahiyo show haikukataliwa tulikubaliana bei lakini hawakurudi tena,”
Post a Comment