Muimbaji wa dancehall, AK47 wa Uganda ambaye ni mdogo wa Jose Chameleone, Weasel na Pallaso amefariki dunia.
Taarfifa zilizoripotiwa na mitandao ya Uganda zinaeleza kwamba Emmanuel Mayanja a.k.a AK47 alifariki usiku wa Jumatatu (March 16) baada ya kuteleza na kudondoka vibaya bafuni.
Alithibitika kuwa amefariki akiwa hospitali ya Nsambya alipokimbizwa na marafiki.
Chameleone na Weasel wakiwa mbele ya mwili wa marehemu AK47
Chameleone aliwataarifu mashabiki wake wa Facebook kwa kuweka tangazo:
“DEATH ANNOUNCEMENT!
Death has robbed us off Emmanuel Mayanja also known as AK 47. To all our friends May God Give us All strength to stand in such a trying time.
My Brother you have Gone too soon.
RIP”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment