0
Inawezekana wewe ni shabiki wa Yamoto Band, lakini ukawa haufahamu kuwa Mh temba wa TMK Wanaume Family ni miongoni mwa watu waliowatengeneza vijana hao ambao mwaka huu wamefanikiwa kwenda Uingereza kufanya show kwa mara ya kwanza. 


Akizungumza kupitia kipindi cha Papaso cha TBC Fm kinachoongozwa na D’Jaro Arungu na kurushwa pia kupitia TBC 1, Temba amesema yeye ni mwanzilishi wa Band hiyo pamoja na Fella.

“Mimi Yamoto Band ndio mwanzilishi na Mkubwa Fella na vile vile ni mshauri wa wale madogo, nasimamia pale nidhamu nasimamia everything, unajua kila mtu anaplay part yake Chambuso kazi yake ni kupokea wageni na kuwasikiliza wanaojua kuimba na wasiojua kuimba, mkubwa Fella as a boss ni the final say, lakini final say anaitoa yeye kwa kupitia kwetu sisi watu wawili mimi na chambuso.”

Temba amezungumza mengi kuhusu muziki wake na kundi la TMK, tazama Interview nzima hapo juu.

Post a Comment

 
Top