0
Ruta Maxmillian Bushoke ni miongoni mwa wasanii waliokuwa busy na show za kampeni zilizodumu kwa miezi miwili.
Kutokana na kutingwa na show hizo, Bushoke alilazimika kusubiri hadi mambo ya uchaguzi yamalizike ili aweze kurejea kikamilifu kwenye muziki.

Bushoke ameiambia Bongo5 kuwa baada ya uchaguzi kumalizika hivi sasa anajipanga kushoot video ya wimbo wake ‘Angel’ aliowashirikisha Mr Blue pamoja na Dullysykes ambao ulitoka mwezi March mwaka huu. Video hiyo itaongozwa na director Eddie Juma.

Kuhusu project mpya, Bushoke amesema kuna wimbo mpya ambao anatarajia kuurekodi siku si nyingi ambao ndio utakuwa official single ambayo hakupenda kuizungumzia zaidi mpaka pale mambo yatakapokaribia kukamilika.

Post a Comment

 
Top