0
Bendi mpya ya vijana wanne, Ruby Band, imezinduliwa rasmi jana pamoja na kutambulishwa kwa video ya wimbo wao mpya ‘Noma’ ndani ya ukumbi wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Vijana wa Ruby Band wakifanya yaoAkizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa bendi hiyo, Deogratius Shija alisema anawaomba wadau na mashabiki wa muziki kuwapokea wasanii hao.


Ruby Band wakiwa na msemaji wa band hiyo, Shija


“Vijana wapo vizuri sana, wadau wapokee video mpya ya wimbo Noma, pia kuna wimbo maalum kwaajili ya kuelisha watu kuhusu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Video ya Noma imeongozwa na Rashid Mrutu,” alisema Shija.

Ruby Band imeundwa na wasanii wanne, Kwea Pipa, Maya Mpogoro, C.Miner pamoja na Sumalay.


Baadhi ya wasanii wa bongo movies


Duma wa Siri ya Mtungi, Shija pamoja na mdau


Vijana wa Ruby Band wakifanya yao



Vijana wakionyesha uwezo wao


Wadau walijitokeza

















Post a Comment

 
Top