Tina akiwa na mwanaye Beyonce mwaka 2013.
Tina na Richard walifunga pingu za maisha katika boti moja la kifahari karibu na ufukwe wa Newport California juzi Jumapili.
Tina akiwa na mumewe wa zamani, Mathew Knowles mwaka 2006. Miongoni mwa waliohudhuria harusi hiyo ni pamoja na binti wa mama huyo, mwanamuziki Beyoncé na mumewe Jay Z pamoja na dada yake Beyonce, Solange Knowles.
Imekuwa ni msimu wa baraka kwa familia ya bi. Tina ambaye mwaka uliopita alishuhudia ndoa ya mwanaye Solange na promota wa muziki, Alan Ferguson.
Tina akiwa na mumewe wa sasa Richard mwaka jana. Haijabainika iwapo baba yao mzazi akina Beyonce ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa Beyonce' bwana Mathew Knowles alikuwepo.
Mathew, 63, aliishi na Tina kwa miaka 31 kati ya mwaka wa 1980 na 2011 na walijaaliwa watoto wawili Beyonce na Solange.
Post a Comment