0
Shetta amekiri kuwa ndoa yake ipo kwenye matatizo hali ambayo inaweza kuvunjika hatua stahili zisipochukuliwa.
Shetta amesema kuwa anaumizwa sana mambo yanayoendelea kuzungumzwa bila ukweli wowote hasa kuhusu uhusiano wake na Rose Ndauka.

“Rose Ndauka ni mshkaji wangu, nilikwenda naye Morogoro kwenye msiba na kukaa naye pamoja na kulala naye hoteli moja ndo limekuwa tatizo,” amesema rapper huyo.

“Watu wanaoanisha sana na haya mambo wakati sio kitu cha ukweli. Inasabisha mambo mengi kutokea kwa upande wangu. Kwa upande wa mke wangu mambo siyo mazuri kidogo siyo sana, mambo siyo mazuri, vitu vinavyoendelea kuzungumza ndo vinaongeza vitu vingine,” alisema Shetta.

Post a Comment

 
Top