0
Muimbaji wa ‘Basi Nenda’ Moshi “Mo Music” Katemi ameweka wazi mapenzi yake kwa muigizaji wa bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.
Mo Music ambaye ametoa wimbo mpya uitwao ‘Nitazoea’ amesema ametokea kumpenda mrembo huyo kutokana na umahiri wa kazi zake za filamu, maana uwezo wake una tofauti kubwa na waigizaji wengine.

Mo Music aliongeza kwamba huwa ana kawaida ya kutazama filamu za wasanii mbalimbali, lakini za Lulu humvutia zaidi kiasi kwamba anatamani ashiriki kama ‘video queen’ katika muziki wake.

“Ninafuatilia kazi za wasanii mbalimbali, ila kwa Lulu ni tofauti, natamani nimshirikishe katika video za wimbo wangu mpya wa ‘Nitazoea’ kwa kuwa naamini ana mvuto mkubwa,” alimaliza Mo Music.

Post a Comment

 
Top