0
Producer na msanii wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel amedai kuwa hajawahi kuondoka na beats za kundi la Pah One alilokuwa mwanzo kama wanavyodai wasanii waliosalia.
Nahreel ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa aliondoka na vitu vyake tu ikiwemo beats ambazo alitengeneza mwenyewe kabla hawajaanzisha kundi ikiwepo beat ya wimbo wa Mwana FA, MfaMle na Pea ambayo alimpa Nick wa Pili.

“Beats zote hizo nilikuwa nazo muda tu niliwaambia kuhusu beats hizo,” alisema.

Katika hatua nyingine Nahreel alisema hakuna mpango wowote wa Navy Kenzo kufanya collabo na Pah One.

Post a Comment

 
Top