0
Chochote ambacho staa mkubwa kama Jay Z akikigusa basi lazima kitageuka kuwa ‘dhahabu’, au kwa lugha nyingine kitaongezeka thamani.
Baada ya rapper na mfanyabiashara Shawn Corey “Jay Z” Carter kuunua mtandao wa ku-stream muziki wa TIDAL kwa dola za Kimarekani milioni 56 mwezi uliopita (March), sasa TIDAL thamani yake imeongezeka na kufikia dola milioni 250, kwa mujibu wa New York Post.

Rapper huyo aliungana na wasanii wenye ushawishi duniani akiwemo Kanye West, Nicki Minaj, J.Cole, Madonna, Beyonce, Alicia Keys, Chris Martin, Usher na wengine kwenye uzinduzi wa TIDAL uliofanyika New York March 30, 2015.

Wasanii hao pia wanatambulika kama waanzilishi wa kampuni huku kila mmoja akiwa na hisa kwenye huduma hiyo.

Post a Comment

 
Top