0
Msanii wa filamu nchini, Ahmed Olotu maarufu kama Mzee Chilo, amesema kuigiza ndani ya filamu ya Going Bongo kumemfunza mambo mengi huku akidai kuwa amegundua filamu nyingi za bongo watu wanakurupuka.

Mzee Chilo (kulia) akiwa na muigizaji mkuu wa filamu ya Going Bongo, Ernest ‘Napoleon’ RwandallaAkizungumza na Bongo5 hivi karibuni katika uzinduzi wa filamu hiyo uliyofanyika Bahari Zoo Tegeta, Mzee Chilo alisema muongozaji filamu hiyo aliwaelekeza waigizaji mambo mbalimbali yaliyowafanya kuwa tayari kisaikolojia kufanya kazi hiyo.


Ernest Napoleon ndio muigizaji mkuu wa filamu hiyo

“Wenzetu wanajipanga wanakuwa na mipango kamili,” alisema. “Siku moja kabla hujaenda ku-shoot wewe umeshaambiwa nguo utakayovaa, sehemu ambayo utafanyia shughuli, nini unatakiwa kusema na nini unatakiwa kujibu yaani unakuwa safi kisaikojia. Halafu kuna watu wanashughulikia wewe kama wewe kuanzia maker-up, mwingine anakushughulikia habari ya nguo, mwingine anahakikisha habari ya vinywaji na chakula, mwingine kama ni sehemu ya nje anahakikisha unalala wapi.

Ina maana wanafanya kila kitu wao hawafanyi kitu kwa kubahatisha. Kama makamera man wote wapo na madirector wao. Sasa nataka na sisi tujifunze tufanye vitu kwa kupangilia tusikurupuke tu. Filamu ya Going Bongo imenifunza. Wengi tunakurupuka na kwa hali hii tutakuwa hatufiki kimataifa kabisa. Kwahiyo mimi nawaambia wasanii watanzania wafunge buti sana tuweze kuwatosheleza watu twende kwa kiwango cha juu sana.”

Post a Comment

 
Top