0
Kitabu cha selfies cha mke wa Kanye West, Kim Kardashian ambacho amekusanya picha zake za selfie na kaziweka kwenye kitabu kimoja kimeuzika kama njugu na kumalizika ndani ya dakika moja.
Kitabu hicho chenye kurasa 352 zenye picha zake za selfie zisizopungua 2,000 kilichopewa jina la ‘Selfish’, kimetoka kwa idadi maalum ya nakala 500 (limited edition copies) ambazo zilisainiwa na Kim K mwenyewe ambazo zimemalizika ndani ya dakika moja toka kilipoanza kuuzwa.

Kupitia Twitter Kim Kardashian amewashukuru mashabiki wake kwa kuandika “Thanks to everyone who got a copy of Selfish on Gilt! Crazy it sold out in one minute!”



Nakala moja imeuzwa kwa $60 (sawa na shilingi 113,000) kila moja kupitia mtandao wa Gilt.com.

Post a Comment

 
Top