0
Ommy Dimpoz amesema mara nyingi mashabiki wa muziki wamekuwa na desturi ya kuzihukumu nyimbo mpya muda mfupi tu baada ya kuzisikia bila kuzipa muda na kuzielewa vyema.

Ommy Dimpoz na mtangazaji wa kipindi cha The Playlist, Lil Ommy wakiwa kwenye studio za Times FM, Jumapili hii Amedai kuwa mara nyingi imetokea kuwa wimbo ulioonekana wa kawaida mwanzoni unakuja kuwa mkubwa baada ya muda kupita.

Ommy amesema katika maisha yake ya muziki hatokuja kusahau jinsi mtu anayemfahamu alipoukosoa wimbo wake wa pili kutoka ‘Baadaye’ kuwa usingefika popote.

Staa huyo anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Wanjera’ alikuwa akiongea Jumapili hii kwenye kipindi cha ‘The Playlist’ cha Times FM na kudai kuwa maoni hayo kupitia Twitter yalimvunja moyo kwa kiasi kikubwa.

Akikumbuka kile kilichoandikwa alisema mtu huyo aliandika kuwa Ommy alianza vizuri na wimbo wake ‘Nai Nai’ aliomshirikisha Alikiba lakini kwa kutoa wimbo ‘Baadaye’ ilionesha jinsi alivyobebwa.

“Ujumbe ule ulinikatisha tamaa sana lakini huwezi kuamini Baadaye ilikuja kuhit na ndio wimbo ulionipa nafasi ya kuanza kwenda kutumbuiza nje,” alisema.

Aliongeza hata wakati anatoa wimbo wake ‘Wanjera’ wengi walioenesha kupenda video na kusema wimbo ni wa kawaida lakini hali imekuywa tofauti.

Ommy aliwataka mashabiki kuzipa kwanza muda nyimbo kabla ya kuzihukumu kama ni mbaya ama nzuri.

Post a Comment

 
Top