Diamond ameshare picha akiwa studio na mapacha hao wa kundi hilo, Peter na Paul Okoye ambayo huenda ni ya wiki kadhaa zilizopita.
“Tafadhali mkiwa Tayari naomba mnambie niiachie, DIAMOND ft P-SQUARE, #MISISAIZIYAKONTAKUPWELEPWETABURE @rudeboypsquare @peterpsquare,” ameandika Diamond.
Si Diamond pekee mwenye furaha na collabo hiyo, bali na P-Square pia.
Peter amepost pia picha hiyo na kuandika: My African people, you asked for it and it’s coming to you soon,” huku Paul akiandika: Hmmmmm…..something is cooking.”
Mashabiki wao wamepokea habari hizo kwa furaha kubwa!
Post a Comment