Madai ya kujeruhi yaliyokuwa yakimkabili Chris Brown jijini Las Vegas yamefutwa.
Polisi wa Las Vegas Jumanne hii wamedai kuwa mtu aliyedai kupigwa ngumi na staa huyo wakati wakicheza basketball ameifuta kesi hiyo ya jinai.
Polisi walisema Brown, 25, alishutumiwa kumpiga mwanaume aliyetibiwa kwenye hospitali ya Sunrise mapema Jumatatu.
Brown alikuwa akicheza kikapu kwenye hoteli aliyofikia na kuanza kurushiana maneno na mtu huyo waliyekuwa wakicheza naye na kuzuka ugomvi wa ngumi. Mtu huyo amedai kuwa alipigwa ngumi na Brown na wakati anajitetea alipigwa na mtu mwingine anayedaiwa kuwa upande wa Brown.
Kwa mujibu wa mtandao wa ThisIs50, Brown alikuwa akicheza kikapu na muimbaji mwenzie Jeremih ambapo baada ya timu ya Jeremih kushinda kukafanyika mechi ya marudiano na ndipo ugomvi ulipozuka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment