0
Said Fella kupitia kampuni yake ya Mkubwa na Wanawe Youth Centre, anawajengea nyumba za kisasa wasanii wanne wa kundi la Yamoto Band na anataka Rais Jakaya Kikwete azizindue!
Kwa mujibu wa Fella nyumba hizo zinazojengwa kwenye eneo moja zitakamilika mwezi July na wasanii hao kukabidhiwa kila mmoja ya kwake.

Kupitia post yake ya jana ya Instagram aliyoitumia kumpongeza Aslay aliyekuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Fella alisema wazo la wasanii hao kuwa na nyumba zilizojengwa eneo moja lilitolewa na msanii muimbaji huyo mkuu wa Yamoto Band.

“Nilikushauri kusapot wenzio hukubisha mpaka tumetengeneza yamoto band mpaka leo umefunga pini mpaka umewatobolesha wenzako Beka,Maromboso na Enock Bella pia kukitambulisha kituo chetu cha mkubwa na wanawe nchini na kwenginepo duniani,” aliandika Fella.

“Najua kuna wadau wanapenda kujua mpaka sasa umefaidika nini wewe. Napenda kuwafamisha japo hupendagi ulisomeshwa na mkubwa fela na ulipata nyumba ya kwanza 2013 na tangu tuiazishe yamoto band ulitoa wazo ulisema ‘mkubwa kama unavyojua familia tuliopotokea naomba tutengenezee kota zetu zifanane hata tukizeeka tuwakumbuke asante’ wazo lako tumelifanyia kazi ujenzi unafikia mwisho na INSHAALLAH tunafanya mipango mimi na viongozi wenzangu wa mkubwa na wanawe youth centre tumpate mh raisi wetu wa jamhuri ya Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE mwezi wa 7 awakabidhi nyote ya moto band nyumba zenu muhimu tuombe dua INSHAALLAH.”

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top