Peter Tonstad, bosi wa mtandao wa kustream muziki wa Jay Z, Tidal ameacha kazi kwenye kampuni hiyo baada ya kuifanyia kazi kwa miezi mitatu tu.
Alijiunga na Tidal April kushika nafasi ya CEO wa mwanzo Andy Chen.
Tidal iliyozinduliwa tena March mwaka huu, inashindana na huduma zingine za aina hiyo kama Spotify, Deezer na Google Play.
Jay Z aliinunua Tidal baada ya kumiliki kampuni ya Sweden, Aspiro mapema mwaka huu kwa gharama ya dola milioni 56. Wasanii wakubwa akiwemo Beyonce, Madonna, Rihanna na Alicia Keys ni miongoni mwa wamiliki.
Lil Wayne alijiunga nayo hivi karibuni.
Mpaka sasa Tidal ina watumiaji takriban 770,000 tu ukilinganisha na milioni 20 waliopo Spotify.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment