0
Ni miaka saba imepita toka msanii wa R-n-B kutoka Morogoro, Belle 9 aanze kufanya vizuri kupitia hit song yake ya ‘Sumu ya Penzi’, lakini hadi leo 2015 bado anatambulika kama msanii wa ndani (local) sababu hajauepeleka muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania.
Belle 9  ni miongoni mwa maswali ambayo nimemuuliza ni kama anaridhika kuendelea kuwa msanii wa ndani tu, na hiki ndicho alijibu:

“Kila kitu mi naamini hua kinakuja kwa muda wake automatically, kama time ya Belle 9 kuwa International ikifika itakuwa hivyo, kiukweli naridhika kuwa local ndio maana naendelea kufanya kazi nzuri na kiukweli sijutii chochote kuhusiana na hii situation kwasababu sina njia ya kubadilisha.” Alisema Belle 9.

Belle 9 amezitaja sababu kubwa mbili ambazo zinamkwamisha kuianza safari yake ya kwenda kimataifa;

“Kwa mimi binafsi nahisi ni connection ndo kitu ambacho ninakosa, na pia management ambayo iko serious kwasababu nimekuwa kwenye management kipindi cha Sumu ya Penzi, Masogange, toka We ni Wangu mpaka leo hii still niko mwenyewe naendelea kufanya hustle mwenyewe, kwahiyo ni tofauti na wasanii wengine ambao wanausimamizi , yaani sijapata serious management nimekuwa tu na ma agent tu wengi , pia niko na timu yangu kama Belle 9 lakini management serious ambayo inaweza kufanya kazi serious bado sijaipata na ndio kitu naamini kinanichelewesha.” Alimaliza Belle 9.

Post a Comment

 
Top