0
Baada ya Joh Makini kuonja asali sasa ana mpango wa kuchonga mzinga kabisa. Baada ya kupata matokeo chanya kutokana na video ya ‘Nusu Nusu’, rapper huyo wa Weusi anatarajia kwenda Afrika Kusini kufanya video nyingine.

Joh Makini akiwa na AKA
“Kusema kweli nimeuona mwanga mkubwa sana wa muziki wa Hip Hop ya Tanzania kimataifa tofauti hata nilivyokuwa nimetarajia, jinsi ambavyo watu wanarespond hii ngoma (Nusu Nusu) nje ya nchi, ni kitu ambacho yani unajua kuna step ukipiga unakuwa kama mteja, ili uweze ku-maintain hiyo step pale inabidi upambane.” Joh Makini ameiambia Bongo5.

Kutokana na mafanikio hayo Joh Makini amesema muda si mrefu ataenda tena Afrika Kusini kufanya video ya wimbo mpya aliofanya na rapper aitwaye AKA wa Afrika Kusini, ambaye hivi karibuni alikuja Tanzania kutumbuiza katika show ya Zari All-White Party.

“Sasa inabidi niende kufanya video ya ngoma ambayo nimefanya na AKA anytime soon, tulifanya hapa hapa Bongo alipokuja jamaa kwenye show ya Zari All-White Party. Nafikiri ndio ngoma ambayo naenda kushoot lakini ni mapema kusema ndio itafata kwenye audio, naweza nikatoa ngoma nyingine tofauti kwenye audio halafu hiyo niliyofanya na AKA natarajia kuiachia video kwanza. “ aliongeza Joh.

Wimbo wa Joh na AKA unaitwa ‘Don’t Bother’, umetayarishwa na Nahreel, na video itafanywa na director aliyefanya video ya ‘Nusu Nusu’, Justin Campos wa Afrika Kusini.

Post a Comment

 
Top