0
Juma Nature amedai kuwa show yake ya miaka 16 kwenye muziki iliyofanyika wiki iliyopita kwenye viwanja vya Dar Live, Mbagala ni jibu tosha la kuwa bado anapendwa, ana mashabiki na anaweza kufanya show kali.

Juma Nature akitumbuiza kwenye viwanja vya Dar Live.


Nature amesema kuwa ni kutokana na chuki za watu wachache, uwezo wake unasahaulika.

“Japokuwa kuna watu wanaleta figisu figisu kutaka kunishusha kimuziki, najua jibu wamepata,” amesema Nature.

“Weekend iliyopita nimewafundisha watu nini maana ya kuwa mkongwe, hili ni funzo kwa underground wote wajifunze wanatakiwa wafanye nini kwenye muziki wao ili waendelee kuishi kwenye maisha ya watu. Kinachofuata sasa hivi ni tour ya muziki wangu, nitazunguka katika mikoa mbalimbali kuzungumza na mashabiki wangu pamoja na kufanya show, pia kupitia show zangu za mikoani underground watapata nafasi ya kuperform.”

Picha kwa hisani ya Globalpublisher

Post a Comment

 
Top