0
Tanzania imetoka kapa kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 zilizofanyika usiku wa Jumamosi hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, Raymond, Navy Kenzo na Yamoto Band walikuwa wametajwa kuwania tuzo hizo.
Ulikuwa ni mwaka wa Wizkid aliyeibuka na tuzo nyingi zaidi, ikiwemo ya msanii bora wa mwaka. Diamond na Alikiba walikuwa miongoni ma wasanii waliotumbuiza.

Wizkid alikuwa man of the night
“Shukran sana sana kwa Kura na support Kubwa mlionipa na mnayoendelea kunipa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.

“Pia S/O kwa my fellow Tanzanian Artist wote waliobahatika kuchaguliwa… Kuingia tunwengi kwenye MtvAwards ni Ushindi tosha kwa Tanzania…ila wanna congrats my brothers @sautisol for the Best Group award… my hommie @jahprayzah and @wizkidayo ya’ll deserve the Trophies,” ameongeza.

Alikiba amepost picha ya Sauti Sol na kuandika: Congratulations to my brothers @sautisol for The MTV Best Group Winner. You have had a great year and you deserve it.”

Naye Vanessa Mdee amepost picha ya Yemi Alade aliyekuwa akishindana naye kwenye kipengele cha msanii bora wa kike na kuandika: Congratulations to my lady love @yemialade na bado tunaenda #Juu and ALL the winners tonight. Thankyou @mtvbaseafrica for the recognition and your continued efforts to elevate Afrikan Music.Now lets get back to work kids.”

Kwa upande wao, Navy Kenzo wamewapongeza Sauti Sol kwa kuandika: With a Great pleasure we Thank God and all Fans, family, friends and all of our teams,Thank you Everyone for voting and it was a great exposure motivation and challenge towards major Goal…! We also Give thanks to @mtvbaseafrica @mtvbaseafrica For the Nomination and recognition we are very happy with a Great Gratitude. Until next Year. EAST AFRICA #KENYA AND AFRICA AT LARGE LET’S STAND TOGETHER AND SAY CONGRATULATIONS @sautisol @sautisol
@sautisol @sautisol #BESTGROUP #AFRICA.”

Hii ni orodha kamili ya washindi.

Best Live Act – Cassper Nyovest (South Africa)

Best Lusophone –C4 Pedro (Angola)

Legend Award –Hugh Masekela (South Africa)

Best Female Award – Yemi Alade (Nigeria)

Best Francophone Award – Serge Beynaud (Ivory Coast)

Best Group – Sauti Sol (Kenya)

Best Pop & Alternative – Kyle Deutsch& Shekhinah (South Africa)

Best International Act – Drake (United State of America)

Best Male Act – Wizkid (Nigeria)

Listeners Choice – Jah Prayzah (Zimbabwe)

Video of the Year – Youssoupha Niguer Ma Vie (Congo)

Best Collaboration – DJ Maphorisa ft, Wizkid & DJ Bucks (South Africa & Nigeria)

Personality of the Year– Caster Semenya (South Africa)

Best Hip Hop – Emtee (South Africa)

Best New Act – Tekno (Nigeria)

Song of the Year – Patoranking ft, Wande Coal (Nigeria)

Artiste of the Year – Wizkid (Nigeria)

Post a Comment

 
Top