“Nimeamua kufunga ndoa kwani nilikaa muda mrefu peke yangu nikatafakari nikaona siyo kitu kizuri nikiwa kama msichana ambaye nina ‘Inspire’ watu wengi lazima kuna vitu nifanye ili niwe mwanamke kamili, maana ukiwa peke yako mtu anaweza kukuchukulia labda huyu mtu muhuni lakini mimi nimeamua kuwa mke wa mtu. Najua ni kitu kikubwa lakini haitanifanya mimi niache kazi zangu za muziki,” alisema.
“Nimeamua kufunga ndoa sababu nimeona nimepata mtu ambaye tunapendana, ninaendana naye na ninampenda sana.”
Licha ya kuwa muislamu, Kadja amesema atafunga ndoa ya Kikristu.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.