Alikiba asema ‘soon’ ataachia wimbo na video mpya
Msanii wa muziki, Alikiba amesema kuwa baada ya kuona wimbo wa “Mwana”
umefanya vizuri anatarajia kuachia wimbo mpya ambao utakuja pamoja na video.
Kiba amesema hana muda wa kusubiria kama mwanzo, sasa hivi ni ngoma baada ya ngoma.
“Kinachofuata ni kazi kama niliyo wa-promise before, hakuna gape, kwaiyo soon so far hakuna gape, lakini muda mchache ambao uliokwepo sasa hivi ndo nafanya kazi, ndo niko nafanya kazi sasa hivi nyimbo nyingine inakuja na video, kwahiyo hicho ndo kitu ambacho kinafuata kama nilivyo waambia hakuna gape, kolabo za kimataifa zipo lakini napendaga Kuwa-surprise watu,” alisema Alikiba.
Post a Comment